ATHARI ZA UJIO WA WAARABU TANGANYIKA
ATHARI ZA UJIO WA WAARABU TANGANYIKA
—Watanganyika wengi waliuwawa zaidi wakati wakishindania uhuru wao. wengi walivikwa minyororo wakauzwe ughaibuni katika nchi ambazo hawana nasaba nazo
—Maelfu walianza kupandikizwa kuchukia ustaarabu wao na hata mwonekano wao wa asili kana kwamba ni watu duni na wenye daraja lisilofaa. Hivyo walijengewa kujichukia si tu katika mwonekano hata katika tamaduni na majina yao waliitwa washenzi.(yaani watu karibu na hayawani katika ufahamu)
—Kuanza kupotea kwa majina asili na kuona kuwa ili upatane na kiwango cha mgeni, basi hata majina wakawa wakiwapa watoto sawa na mgeni aliyewatawala wakidhani katika hayo wangepata ahueni lakini pia wangeweza kuwa kama wageni.
—Watanganyika wengi walipokuwa wakiuzwa kama watumwa walipokuwa wamezidi katika Mshua walikuwa wakipunguzwa kwa kutupwa kama bidhaa nyingine Baharini ili kuepusha chombo kuzama majini.
Comments
Post a Comment