WAADHI: WATESI —Papa aliyeamuru kufanywa watumwa kwa watu kulingana na rangi zao. —Aliwaambia Wareno kuwaendea watu weusi na kuwafanya watumwa. —Papa huyu aliitwa Nikolasi V alileta ubaguzi na ndiye aliyewafukuza Wamua {Moers} kupitia kanisa aliwafanya waafrika watumwa kutokana na weusi wao. —Papa Nicholas V alitoa waraka ujulikanao kama " papal bull Dum Diversas mnamo 18 June 1452". Uliomruhusu Alfonso V wa ureno kupuwapunguza "Waislamu na Wapaganina wale wote wasio waamini" kwa kuwafanya watumwa na hili lilichochea biashara ya utumwa kwa wareno kuja afrika ya magharibi na kuwafanya waafrika watumwa. +Papa huyuhuyu ndiye aliyeandika waraka uitwao "bull Romanus Pontifex" Mnamo Januari 5, 1455, Kwenda kwa Alfonso. Kama waraka unaotaka mrejesho wa waraka wa awali " Dum diversas". Si tu ulitakasa uporwaji wa ardhi za wakazi asilia wasiokuwa Wakristo, lakini ulihamasisha kufanywa watumwa kwa wazawa wa ardhi hususa ambao hawakuwa wakristo bara...
WAADHI: NDOA YA WAKHOSA —Jamii ya wakhosa au kabila la Wakhosa linapatikana jamhuri ya Afrika ya kusini. +Kuna takribani Wakhosa milioni 8 nchini Afrika kusini. Katika jadi upande wa mwanamume ndiyo humchagulia mtoto wao mwenzi wakuoa. Ndipo tendo la "Ukutwala" neno sawia na wazungumzaji wa lugha ya kinyakyusa lenye maana ya "Kutwaa au kuchukua/kuleta" hufanywa. —Ndoa hii ya jadi inajulikana kama "Ukwenda" yumkini wazungumzaji wa lugha ya kinyakyusa wakawa wanashangaa kufanana kwa maneno haya na kuwa na maana sawa {Tutazungumzia wakati mwingine} +Sherehe ya "ukwenda" inachukua yapata siku mbili katika jadi ya kabila hili na huusisha jamii yote ya karibu. +Baadhi ya nyama hutolewa kwa mababu kama kafara. Ndoa za jadi za kabila hili huusisha Ibada nyingi kwa kweli ni zenye kuvutia na kuonesha utajiri wao katika ustawi wa jamii hii. —NAIPENDA AFRIKA
ATHARI ZA UJIO WA WAARABU TANGANYIKA —Watanganyika wengi waliuwawa zaidi wakati wakishindania uhuru wao. wengi walivikwa minyororo wakauzwe ughaibuni katika nchi ambazo hawana nasaba nazo —Maelfu walianza kupandikizwa kuchukia ustaarabu wao na hata mwonekano wao wa asili kana kwamba ni watu duni na wenye daraja lisilofaa. Hivyo walijengewa kujichukia si tu katika mwonekano hata katika tamaduni na majina yao waliitwa washenzi.(yaani watu karibu na hayawani katika ufahamu) —Kuanza kupotea kwa majina asili na kuona kuwa ili upatane na kiwango cha mgeni, basi hata majina wakawa wakiwapa watoto sawa na mgeni aliyewatawala wakidhani katika hayo wangepata ahueni lakini pia wangeweza kuwa kama wageni. —Watanganyika wengi walipokuwa wakiuzwa kama watumwa walipokuwa wamezidi katika Mshua walikuwa wakipunguzwa kwa kutupwa kama bidhaa nyingine Baharini ili kuepusha chombo kuzama majini.
Kazi nzuri sana karibuni
ReplyDelete