WAADHI: WATESI —Papa aliyeamuru kufanywa watumwa kwa watu kulingana na rangi zao. —Aliwaambia Wareno kuwaendea watu weusi na kuwafanya watumwa. —Papa huyu aliitwa Nikolasi V alileta ubaguzi na ndiye aliyewafukuza Wamua {Moers} kupitia kanisa aliwafanya waafrika watumwa kutokana na weusi wao. —Papa Nicholas V alitoa waraka ujulikanao kama " papal bull Dum Diversas mnamo 18 June 1452". Uliomruhusu Alfonso V wa ureno kupuwapunguza "Waislamu na Wapaganina wale wote wasio waamini" kwa kuwafanya watumwa na hili lilichochea biashara ya utumwa kwa wareno kuja afrika ya magharibi na kuwafanya waafrika watumwa. +Papa huyuhuyu ndiye aliyeandika waraka uitwao "bull Romanus Pontifex" Mnamo Januari 5, 1455, Kwenda kwa Alfonso. Kama waraka unaotaka mrejesho wa waraka wa awali " Dum diversas". Si tu ulitakasa uporwaji wa ardhi za wakazi asilia wasiokuwa Wakristo, lakini ulihamasisha kufanywa watumwa kwa wazawa wa ardhi hususa ambao hawakuwa wakristo bara...
ATHARI ZA UJIO WA WAARABU TANGANYIKA —Watanganyika wengi waliuwawa zaidi wakati wakishindania uhuru wao. wengi walivikwa minyororo wakauzwe ughaibuni katika nchi ambazo hawana nasaba nazo —Maelfu walianza kupandikizwa kuchukia ustaarabu wao na hata mwonekano wao wa asili kana kwamba ni watu duni na wenye daraja lisilofaa. Hivyo walijengewa kujichukia si tu katika mwonekano hata katika tamaduni na majina yao waliitwa washenzi.(yaani watu karibu na hayawani katika ufahamu) —Kuanza kupotea kwa majina asili na kuona kuwa ili upatane na kiwango cha mgeni, basi hata majina wakawa wakiwapa watoto sawa na mgeni aliyewatawala wakidhani katika hayo wangepata ahueni lakini pia wangeweza kuwa kama wageni. —Watanganyika wengi walipokuwa wakiuzwa kama watumwa walipokuwa wamezidi katika Mshua walikuwa wakipunguzwa kwa kutupwa kama bidhaa nyingine Baharini ili kuepusha chombo kuzama majini.
Kazi nzuri sana karibuni
ReplyDelete