WAADHI: NDOA YA WAKHOSA
WAADHI: NDOA YA WAKHOSA
—Jamii ya wakhosa au kabila la Wakhosa linapatikana jamhuri ya Afrika ya kusini.
+Kuna takribani Wakhosa milioni 8 nchini Afrika kusini. Katika jadi upande wa mwanamume ndiyo humchagulia mtoto wao mwenzi wakuoa. Ndipo tendo la "Ukutwala" neno sawia na wazungumzaji wa lugha ya kinyakyusa lenye maana ya "Kutwaa au kuchukua/kuleta" hufanywa.
—Ndoa hii ya jadi inajulikana kama "Ukwenda" yumkini wazungumzaji wa lugha ya kinyakyusa wakawa wanashangaa kufanana kwa maneno haya na kuwa na maana sawa {Tutazungumzia wakati mwingine}
+Sherehe ya "ukwenda" inachukua yapata siku mbili katika jadi ya kabila hili na huusisha jamii yote ya karibu.
+Baadhi ya nyama hutolewa kwa mababu kama kafara. Ndoa za jadi za kabila hili huusisha Ibada nyingi kwa kweli ni zenye kuvutia na kuonesha utajiri wao katika ustawi wa jamii hii.
—NAIPENDA AFRIKA
Comments
Post a Comment