Posts

ATHARI ZA UJIO WA WAARABU TANGANYIKA

 ATHARI ZA UJIO WA WAARABU TANGANYIKA —Watanganyika wengi waliuwawa zaidi wakati wakishindania uhuru wao. wengi walivikwa minyororo wakauzwe ughaibuni katika nchi ambazo hawana nasaba nazo  —Maelfu walianza kupandikizwa kuchukia ustaarabu wao na hata mwonekano wao wa asili kana kwamba ni watu duni na wenye daraja lisilofaa. Hivyo walijengewa kujichukia si tu katika mwonekano hata katika tamaduni na majina yao waliitwa washenzi.(yaani watu karibu na hayawani katika ufahamu) —Kuanza kupotea kwa majina asili na kuona kuwa ili upatane na kiwango cha mgeni, basi hata majina wakawa wakiwapa watoto sawa na mgeni aliyewatawala wakidhani katika hayo wangepata ahueni lakini pia wangeweza kuwa kama wageni.  —Watanganyika wengi walipokuwa wakiuzwa kama watumwa walipokuwa wamezidi katika Mshua walikuwa wakipunguzwa kwa kutupwa kama bidhaa nyingine Baharini ili kuepusha chombo kuzama majini.

WAADHI: MAATI

 WAADHI: MAATI Umewahi kustaajabia ulimwengu na nafasi yako katika ulimwengu? —Umewahi kutizama nyota na kuhisi kuunganika na kitu kikubwa zaidi kuliko wewe mwenyewe!? —Ikiwa ndivyo na unapendezwa na utafutaji wako wa hekima basi Italia vyema ukafuatilia mafundisho ya kitabu cha kale cha Misri sahihi ambayo haikuchafuliwa na waarabu au wazungu kwa kusoma kitabu kiitwacho MAAT. —Kila jumapili tutakichunguza mstari kwa mstari na historia mbalimbali kuhusiana nacho na jinsi Misri ya kale au KEMETI ilivyokuwa yenye ustaarabu kabla ya kuvamiwa na wagiriki, waingereza na hata waarabu ambao mpaka SASA wamekuwa wengi kuliko waliokuwa wazawa. Nuru na ituangaze.

WAADHI: WATESI

 WAADHI: WATESI —Papa aliyeamuru kufanywa watumwa kwa watu kulingana na rangi zao. —Aliwaambia Wareno kuwaendea watu weusi na kuwafanya watumwa. —Papa huyu aliitwa Nikolasi V alileta ubaguzi na ndiye aliyewafukuza Wamua {Moers} kupitia kanisa aliwafanya waafrika watumwa kutokana na weusi wao.   —Papa Nicholas V alitoa waraka ujulikanao kama " papal bull Dum Diversas mnamo 18 June 1452".  Uliomruhusu Alfonso V wa ureno kupuwapunguza "Waislamu na Wapaganina wale wote wasio waamini" kwa kuwafanya watumwa na hili lilichochea biashara ya utumwa kwa wareno kuja afrika ya magharibi na kuwafanya waafrika watumwa. +Papa huyuhuyu ndiye aliyeandika waraka uitwao "bull Romanus Pontifex" Mnamo Januari 5, 1455, Kwenda kwa Alfonso. Kama waraka unaotaka mrejesho wa waraka wa awali " Dum diversas". Si tu ulitakasa uporwaji wa ardhi za wakazi asilia wasiokuwa Wakristo, lakini ulihamasisha kufanywa watumwa kwa wazawa wa ardhi hususa ambao hawakuwa wakristo bara...

WAADHI: NDOA YA WAKHOSA

 WAADHI: NDOA YA WAKHOSA —Jamii ya wakhosa au kabila la Wakhosa linapatikana jamhuri ya Afrika ya kusini. +Kuna takribani Wakhosa milioni 8 nchini Afrika kusini. Katika jadi upande wa mwanamume ndiyo humchagulia mtoto wao mwenzi wakuoa. Ndipo tendo la "Ukutwala" neno sawia na wazungumzaji wa lugha ya kinyakyusa lenye maana ya "Kutwaa au kuchukua/kuleta" hufanywa. —Ndoa hii ya jadi inajulikana kama "Ukwenda" yumkini wazungumzaji wa lugha ya kinyakyusa wakawa wanashangaa kufanana kwa maneno haya na kuwa na maana sawa {Tutazungumzia wakati mwingine} +Sherehe ya "ukwenda" inachukua yapata siku mbili katika jadi ya kabila hili na huusisha jamii yote ya karibu. +Baadhi ya nyama hutolewa kwa mababu kama kafara. Ndoa za jadi za kabila hili huusisha Ibada nyingi kwa kweli ni zenye kuvutia na kuonesha utajiri wao katika ustawi wa jamii hii. —NAIPENDA AFRIKA

UFALME WA MUTAPA

 Dondoo: UFALME WA MUTAPA  +Ufalme au Dola ya Mwanamutapa/Mutapa ilienea haswa kusini mwa Afrika kuanzia Limpopo na MTO Zambezi mpaka kufika Bahari ya Hindi. +Dola hii ilijumuisha kile kiitwacho wakati wa Leo nchi ya Lesotho, Jamhuri ya Afrika kusini, Msumbiji, Zambia, Eswatini pamoja na Zimbabwe. +Fikiria namna dola hii ilivyopata kuwa kubwa zaidi wakati huo au ingekuwa kubwa kiasi gani kwa wakati wa leo. +Inaaminika kulingana na simulizi kuwa Mwanamfalme Nyatsimbe kutoka ufalme wa Zimbabwe ndiye aliyeasisi ufalme wa Mutapa yapata karne ya 15, akichukua madaraka kutoka kwa Babu yake Mbire ambaye aliianzisha KAZI hususa yapata Karne ya 14. +Biashara baina ya Ufalme wa Mutapa na India ilikuwa katika ustawi mkubwa Sana. +Dola hii ilivamiwa na Wareno walioingia wakitokea pwani ya mashariki yapata miaka ya 1530 wakati mwene Mutapa aliposubutu kuwafukuza mnamo 1629.

THIS IS ARUSHA TANZANIA

Arusha 🇹🇿  Arusha is a city in northern Tanzania, situated at the base of Mount Meru. It is the capital of the Arusha Region and serves as the gateway to the popular safari destinations of Serengeti National Park, Ngorongoro Conservation Area, Tarangire National Park, and Lake Manyara National Park. Arusha is also known as the "Safari Capital of Tanzania" and is a significant international diplomatic hub, hosting the East African Community (EAC) headquarters and various international organizations. The city has a pleasant climate due to its elevation and is a starting point for many tourists embarking on safaris in the region. Additionally, Arusha has a diverse cultural scene, with various ethnic groups residing in the area, including the Maasai, Meru, and Arusha people. The city also has markets, museums, and cultural heritage sites that showcase the rich history and traditions of the region.  Welcom to my blog 

Karibuni kwenye blog yangu mpya ntakuwa nawaletea habari za michezo na burudani

 Karibuni kwenye blog yangu mpya ntakuwa nawaletea habari za michezo na burudani